Friday, July 3, 2015

FOMU YA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO SHULENI ENGUTOTO 2015

halmashauri ya wilaya ya monduli MKOA WA ARUSHA ENGUTOTO SEKONDARI Barua zote ziandikwe kwa: S.L.P 143 Simu Na:+255 754 205 853. +255 754 859 146 MONDULI 03.06.2015 Unapojibu tafadhali taja: KUMB. NA: ENG/SS/F5.SEL/2015/01 NDUGU MZAZI/MLEZI WA …………………………………………………………. SHULE ATOKAYO……………………………………………………………... YAH: MAAGIZO YA KUJIUNGA NA SHULE KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO 2015 “JOINING INSTRUCTIONS “ 1.0. UTANGULIZI: Ndugu Mzazi/Mlezi, ninayo furaha kukutaarifu kuwa, mwanao amechaguliwa kujiunga na kidato cha V~ 2015 (HGL/HKL /HGK) katika shule ya sekondari ENGUTOTO. Nitumie nafasi hii, kukupongeza wewe na mwanao kwa kupata bahati hii, ambayo watu wengi wameikosa. HONGERA KWA KUCHAGULIWA NA KARIBU SANA katika shule ya sekondari ENGUTOTO kwa ajili ya kupata ELIMU BORA. Ni matumaini yangu kuwa, mwanao ataitumia nafasi hii vizuri kwa manufaa yake binafsi, familia na Taifa kwa ujumla. Shule ya sekondari ENGUTOTO, ipo mjini MONDULI mkabala na kituo cha Mafuta GAPCO, ambacho pia ni kituo cha Mabasi maarufu kwa jina la “SHELI” kilichopo katika barabara kuu ya ARUSHA ~ MONDULI. Shule ya sekondari Engutoto, ni ya BWENI kwa kidato cha 1 hadi cha 6. 2.0.Shule itafunguliwa rasmi siku ya Jumatatu tarehe 06/07/2015 na mwanafunzi anatakiwa afike siku hiyo kabla ya saa 9:00 mchana bila kukosa, akiwa ameambatana na Fomu zote zilizoambatanishwa na barua hii, zikiwa zimejazwa kikamilifu na wahusika na kuzikabidhi shuleni wakati wa usajili. 3.0. Vifaa/Mahitaji ya lazima unayotakiwa kumkamilishia mwanao ni kama ifuatavyo: 3.1. SARE ZA SHULE. 3.1.1 WAVULANA: I. Suruali 2 za heshima rangi ya kahawia zenye marinda. II. Shati 3 za heshima rangi nyeupe mikono mirefu, III. Viatu vya ngozi rangi nyeusi SIO BUTI vya kamba na visiwe na kisigino kirefu. IV. Suruari moja ya heshima rangi ya kijivu kwaajili ya kuvaa siku ya kwenda msikitini au kanisani. V. Soksi jozi mbili rangi nyeusi , VI. Mkanda mweusi wa kawaida usio na urembo. VII. Sweta ya rangi bluu bahari inapatikana shuleni kwa bei ya Tshs 17,000/= VIII. Jezi za michezo zinapatikana shuleni kwa bei ya Tshs. 15,000/= IX. Tai rangi ya kahawia X. Suruali mbili nyeusi za kushindia, pamoja na shati /T – shirt mbili za light blue. XI. Koti jeusi kwa ajili ya baridi usiku N.B. MARUFUKU KUJA NA NGUO ZA NYUMBANI. 3.2. MAHITAJI MENGINE MUHIMU Kila mwanafunzi alete: (i) Tshs 70,000/= kwa mwaka au 35,000/= kwa mhula kwaajili ya ADA ya shule. (ii) Tshs 5,000/= kwa ajili ya fedha ya Tahadhari. (iii) Tshs 5,000/= kwa ajili ya fedha ya Kitambulisho cha shule. (iv) Tshs 10,000/= kwa ajili ya T shirt ya shule (v) Tshs 40,000/= kwa ajili ya uboreshaji wa Taaluma. (vi) Tshs 40,000/= kwa ajili ya uboreshaji wa miundo mbinu (vii) Tshs 15,000/= kwa ajili ya matibabu. (viii) Tshs 2,000/= kwa ajili ya Nembo ya shule (ix) REKI 1 na PANGA 1 jipya lenye mpini, (x)Daftari kubwa counter Quire( 4) 7, rula ndefu (futi moja) kalamu za wino, penseli na mkebe (Mathematical Set), (xi) Mfuko (School bag ) mzuri na imara kwa ajili ya kubebea vitabu na daftari za shule , (xii) Shuka mbili za rangi ya pink (xiii) Ndoo mbili kwaajili ya kuhifadhia maji yake ya kunywa na kuogea. (xiv) Sanduku la bati kwa ajili ya kutunzia vitu vyake kwa usalama zaidi. (xv)SAHANI, KIKOMBE na KIJIKO kwa ajili ya chakula chake, Vyombo Hivyo visiwe vya Plastiki. Ni MARUKUKU kwa mwanafunzi yeyote Kuchangia vyombo wakati wa kula (Xvi) Kila mwanafunzi aje na “RIM” (rulled paper) moja ya karatasi kwa ajili ya mitihani na majaribio. N.B: kila mwanafunzi aje na godoro, futi tatu(3) 3.3. Ndugu Mzazi/Mlezi, Jumla ya Fedha yote unayopaswa kumlipia mwanao ni Tshs 187,000 /=kwa mwaka au Tshs 152,000/=kwa muhula wa kwanza. Ili aweze kusajiliwa Fedha hiyo ilipwe katika Tawi lolote la Benki ya NMB kabla mwanafunzi hajaripoti shuleni. Jina la Akaunti ni “ENGUTOTO SECONDARY SCHOOL FUND “ Namba ya Akaunti ni 41301100030. Mwanafunzi atakaporipoti shuleni, ni lazima awasilishe nakala ya BANK PAY-IN SLIP (BPS), ikionyesha wazi, jina kamili la mwanafunzi huyo na sio jina la Mzazi/Mlezi. FEDHA ZA SWETA TSHS. 17,000/= NA JEZI TSHS. 15,000/= ZILETWE SHULENI MOJA KWA MOJA SIO KULIPIA BENKI. 4.0. MAKOSA YANAYOWEZA KUSABABISHA MWANAFUNZI KUFUKUZWA SHULE: (i) Wizi wa aina yoyote, (ii) Uasherati, Ubakaji, Ulawiti na Ushoga, (iii) Ulevi na matumizi ya dawa za kulevya, (iv) Uvutaji wa bangi, (v) Makosa ya Jinai, (vi) Kupiga au kupigana, (vii) Kuharibu kwa makusudi mali ya mtu/shule /Umma/ fedha za Serikali (viii) Kudharau bendera ya Taifa /Viongazi wa Serikali, (ix) Kuoa (x) Kusababisha mimba nje ya shule (xi) Kutohudhuria vipindi vya darasani, ikiwa ni pamoja na vipindi Viwili vya Dini kila wiki, kutofanya mitihani, majaribio au kazi nyingine za shule bila kibali cha Mkuu wa shule (xii) Kugoma, kuchochea na kuongaza mgomo au kuvuruga amani na usalama wa shule,raia na mali zao, (xiii) Ushabiki wa vyama vya siasa ukiwa shuleni, (xiv) Kuvunja sheria za shule (xv) Kukataa adhabu ya viboko. (xvi) Ni marufuku mwanafunzi kuja na SIMU YA MKONONI SHULENI. Ukikutwa na simu itavunjwa vunjwa mara moja na utafutwa shule bila onyo ya awali. 5.0. MUHIMU SANA KWA MWANAFUNZI NA MZAZI/MLEZI: i. Mwanafunzi hatapokelewa shuleni kama hakukamilisha kipengele cha 2.0 na 3.0 hapo juu, ii. Mwanafunzi afike shuleni akiwa na nakala ya “result slip” ya kidato cha nne kuepuka usumbufu katika usajili. iii. School Motto ni “ EDUCATION FOR WISDOM” (ELIMU KWA AJILI YA KUPATA BUSARA), HITIMISHO: Ikiwa Mzazi/Mlezi na mwanafunzi HAKUBALIANI na MASHARTI yaliyotajwa katika maagizo haya, mwanafunzi ASIJE SHULENI na MZAZI/MLEZI afanye utaratibu wa kumtafutia UHAMISHO kijana wake kwenda shule nyingine itakayomfaa. Mwanafunzi anayeamua kuja hapa shuleni, baada ya kusoma na kuelewa taratibu za shule hii ya sekondari Engutoto, hategemewi kuvunja Sheria / Kanuni na Taratibu za Shule, kwani akifanya hivyo ni kwa makusudi na sio bahati mbaya. Mwisho, Karibu sana Shule ya Sekondari ENGUTOTO ili ufaidike kwa kupata ELIMU BORA. …………………… MKUU WA SHULE Nakala: (i) Katibu Mkuu ~ WEMU …………………. Kwa Taarifa (ii) Afisaelimu (M) …………………. Kwa Taarifa (iii) Mkaguzi Mkuu wa Shule (K) ………………….. Kwa Taarifa (iv) Afisaelimu shule za sekondari (W) MONDULI …… Kwa Taarifa (v) Wajumbe wa Bodi ya Shule ~ Engutoto Sekondari ... Kwa Taarifa WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI SHULE YA SEKONDARI ENGUTOTO TAARIFA MUHIMU ZA MWANAFUNZI FOMU A SEHEMU HII IJAZWE NA MWANAFUNZI MWENYEWE KWA HERUFI KUBWA: 1. (i) JINA LA MWANAFUNZI ………………………………………………… NB: Jina liwe lile lililotumika katika mtihani wa kidato cha nne - 2014. (ii) Tarehe ya kuzaliwa ………………… kijiji …………………… kata …………… Tarafa ……………………….. Wilaya ……………………….. Mkoa…………… (iii) Dini ………………………………………… Madhehebu ………………………. 2. AFYA: (i) Taja magonjwa yoyote makubwa uliyowahi kuugua k.m.f. TB, POLIO, KIFAFA n.k. ………………………………………………………………………………………… (ii) Taja matatizo yoyote ya afya yako ………………………………………………….. 3. JINA LA MZAZI: (i) Baba …………………………………………. Hai/ Amefariki Lini ………….... (ii) Mama ………………………………………… Hai/ Amefariki Lini ………………. ( Kata isiyostahili) 4. KAZI YA: (i) Baba ……………………… Dini ………………… Madhehebu …......................... (ii) Mama …………………….. Dini …………………. Madhehebu …………………. (iii) Anwani ya Mzazi/Mlezi ………………………………………………………….... (iv) Mwanafunzi anaishi na: (Weka V sehemu iliyo sahihi) (a) Baba tu (b) Mama tu (c) Wazazi wote wawili (d) Mlezi 5. MZAZI/MLEZI/TAASISI ITAYOGHARAMIKIA MAHITAJI YA SHULE: (i) Jina …………………………………………………………………………………. (ii) Kazi yake ni ………………………………………………………………………… (iii) Anuani yake ni ………………………...... (iv) Simu …………………………….. (v) Uhusiano wake …………………………. (Mf. Baba, Mama, Dada, Mjomba n.k) (iv) Dini yake …………………………...... Madhehebu ………………………………. 6. UTHIBITISHO WA MWANAFUNZI: Mimi ……………………………….. nakubali kujiunga na Shule ya ENGUTOTO Sekondari na kuthibitisha kuwa, nitafuata sheria na Taratibu zote za Shule hii ili nitimize lengo la kuja shuleni kwa manufaa yangu/ familia na Taifa kwa ujumla. Endapo nitakwenda kinyume na Sheria /Kanuni /Taratibu za shule nitakubali kuadhibiwa. Saini ya mwanafunzi ………………………………. Tarehe ……………………………. 7. SEHEMU HII IJAZWE NA MZAZI/MLEZI/TAASISI HUSIKA: Mimi ……………………………………. Nathibitisha kuwa, taarifa hiyo hapo juu ni sahihi. Ninaahidi kushirikiana na uongozi wa shule na walimu wote kuhakikisha kijana wangu anakuwa na NIDHAMU na JUHUDI katika masomo. Aidha, nitagharamia Mahitaji yake ya shule, ili kumjengea mazingira mazuri ya kusoma katika kipindi chote atakachokuwa shuleni kwa kuzingatia sheria/ Kanuni na Taratibu za Shule. Saini ya Mzazi/Mlezi/Taasisi ……………………………….. Tarehe …………… MINISTRY OF EDUCATION AND VOCATIONAL TRAINING FORM B part A ENGUTOTO SECONDARY SCHOOL P.O.BOX 143 TEL: +255 754 205 853 / +255 754 859 146 MONDULI 03.06.2015 REF.NO:ENG/SS/F.V.SEL/2015/02 TO: THE MEDICAL OFFICER, ………………………………. ……………………………… RE: REQUEST FOR MEDICAL EXAMINATION TO: Mr. ……………………………………………………… FORM 5~ 2015 Please examine the above named as to his physical and mental fitness for full time schooling course. The Examination should include the following categories [i-iii]. (i) (a) Eye (b) Hearing (c) Limbs (d) Speech (e) Venereal disease (s) (f) Leprosy (g) Epilepsy (ii). Neuroses (iii)Other serious diseases ………………………… HEADMASTER PART B. MEDICAL CERTIFICATE [To be completed by Government Medical Officer] I have examined the above named and consider that * he is physically * fit/unfit and mentally * fit/unfit for the full time schooling course: (i) (a) Eye Sight ……………………………. (b) Hearing …………...................... (c) Limbs ………………………………. (d) Speech …………………………. (e) Venereal diseases (s) …………………. (f) Leprosy ……………………….. (g) Epilepsy ………………………………….. (ii)Neuroses ………………………………………………………. (iii) Other serious diseases ………………………………………… Station ………………………………………………. Signature ……………….............. Designation ……………………………………………. Date …………………………. * Delete whichever is unnecessary.